Mbelgiji Ashindwa Kuamua Vita ya Bwalya, Chama

4 0Mbelgiji Ashindwa Kuamua Vita ya Bwalya, Chama

KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck, amesema kuwa kutokana na ubora wa viungo wake, hivi sasa ana uhakika wa kumpanga kiungo yeyote katika kikosi chake.

 

Hiyo ni baada ya timu hiyo kukamilisha usajili wa kiungo bora hivi sasa nchini Zambia, Larry Bwalya aliyejiunga na timu hiyo hivi karibuni katika kuelekea msimu mpya wa 2020/2021.

 

Kutua kwa kiungo huyo kunafikisha idadi ya viungo nane katika timu hiyo wengine ni Clatous Chama, Francis Kahata, Ibrahim Ajibu, Hassani Dilunga, Jonas Mkude, Gerson Fraga, Said Ndemla na Mzamiru Yassin.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Sven alisema kuwa kila kiungo ana nafasi ya kucheza katika kikosi kutokana na timu anayokutana nayo, kikubwa ni mchezaji anatakiwa kuonyesha kiwango kikubwa kwa kila mchezo atakaoucheza ili apate nafasi zaidi ya kucheza katika michezo inayofuata.

 

Sven alisema kuwa kati ya safu ambazo zipo vizuri ni ya kiungo tangu msimu uliopita, lakini ujio wa Bwalya umeimarisha kikosi chake kutokana na uwepo wa viungo wengi, hali inayomfanya yeye amtumie mchezaji yeyote aliye kwenye ubora.

 

Aliongeza kuwa katika msimu huu, ana uhakika wa kumpanga mchezaji endapo mmoja atakuwa mgonjwa au anatumikia adhabu ya kadi, hivyo hatapata wakati mgumu wa kuumiza kichwa.

“Ujio wa Bwalya utaimarisha kikosi changu katika kuelekea msimu ujao, hiyo ni baada ya kukamilisha usajili wa kiungo huyo bora hivi sasa nchini Zambia.

 

“Bwalya ataongeza ushindani wa namba katika kikosi changu, kwani kila mmoja atatumia nafasi atakayoipata kuonyesha uwezo wake ili kuhakikisha anapata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

Wilbert Molandi, Dar es SalaamToa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *