Mbelgiji Yanga Amzungumzia Straika wa Sweden

27 0Mbelgiji Yanga Amzungumzia Straika wa Sweden

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mbelgiji, Luc Eymael amekiri kumfanyia majaribio mshambuliaji wa timu ya IFK Östersund inayoshiriki Ligi Daraja la Pili ya Sweden, Yusuph Soka.

 

Soka ni Mtanzania ambaye alikuwa pacha wa mshambuliaji wa Aston Villa, Mtanzania, Mbwana Samatta wakati wakiwa African Lyon kabla ya kutimkia Ulaya ambapo inaelezwa alibadili uraia na kuchukua uraia wa Sweden.

 

Mshambuliaji huyo kwa sasa yupo nchini akifanya mazoezi na timu hiyo kwa siku moja kabla Yanga kuelekea Morogoro kucheza na Mtibwa Sugar katika mchezo uliopigwa juzi Jumatano na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Eymael alisema lengo la kumpa nafasi ya kufanya mazoezi na timu hiyo ni kuangalia uwezo wake kabla ya kumpa mkataba wa kuitumikia timu hiyo.

 

“Ni kweli huyo mchezaji tulifanya mazoezi naye siku moja kabla ya kuanza safari ya mechi zetu mbili za kumaliza ligi, nimempa nafasi kwa sababu nataka kumsajili lakini bado anahitaji muda zaidi wa kumuangalia uwezo wake.

 

“Unajua ni mara ya kwanza nimemuona baada ya kupewa taarifa na amefanya na sisi mazoezi kwa siku moja pekee, haiwezi kutoa majibu kwa sababu nataka kumpa muda zaidi hapo baadaye ili kuweza kujiridhisha kwa kile ambacho nahitaji kuamua juu yake,” alisema Eymael.

Ibrahim Mussa na Abdulghafal AllyToa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *