Mbelgiji Yanga: Huyu ndiye Fei Toto ninayemtaka

BAADA ya kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’, kuonyesha kiwango bora katika mchezo uliopita dhidi ya Alliance, kocha mkuu wa timu hiyo, Luc Eymael, amekoshwa na uwezo wa nyota huyo na kusema kuwa anatamani kumuona nyota huyo akicheza hivyo kila siku.

 

Yanga katika mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar, walifanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 2-0, yote yakifungwa na Ditram Nchimbi.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, kocha huyo alisema kuwa amefurahishwa na uwezo wa mchezaji huyo huku akitamani kila mechi acheze kwenye uwezo mkubwa kama ambao ameuonyesha dhidi ya Alliance.

 

“Feisal ni mchezaji mzuri sana na ana kipaji kikubwa pia, ukimuangalia mazoezini basi utamgundua ni mchezaji wa aina gani, kuna vitu vidogo sana vilikuwa vinamfanya ashindwe kufanya vizuri, nadhani kwa sasa vimemalizika na unaona jinsi ambavyo amecheza vizuri, hakika natamani acheze hivi kila siku,” alisema kocha huyo.

 

Feisal tangu kuondoka kwa kocha wa zamani wa timu hiyo, Mwinyi Zahera, amekuwa akikosa nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo huku katika nafasi yake mara nyingi amekuwa akitumika kiungo Papy Tshishimbi.

MARCO MZUMBE, Dar es Salaam
Toa comment