Mbio za NMB Bima Marathon!

12 0

Benki ya NMB inatarajia kukusanya zaidi ya Sh. milioni 100 kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye saratani katika
mbio za NMB Bima Marathon zilizopangwa kufanyika Septemba 12 jijini Dar es Salaam.

 Fedha hizo zinatarajia kupatikana kupitia kwenye ada ya ushiriki wa mashindano hayo kwa upande wa Kilometa 5
ambazo zitashirikisha wadau mbalimbali watakaojitokeza kushiriki katika mbio hizo zilizopangwa kuanzia jengo la
Mlimani City.

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB – Filbert Mponzi alisema kuwa
wanatarajia  kushirikisha jumla ya wanariadha 3,000 katika mbio hizo ambazo zimeandaliwa na kampuni ya The
Africa Digital Banking Summit inayoongozwa na Baraka Mtavangu.

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB – Filbert Mponzi akizungumza wakati wa Mkutano na
Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na Mbio za NMB Bima Marathon zitakazofanyika Jumamosi ijayo.
Kushoto ni Mwakilishi wa waandaaji wa mbio hizo – Baraka Mtavangu na Mwakilishi kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili – Dkt. Rehema Laiti.

Mponzi alisema kuwa, viingilio vyote vya mbio za kilometa 5 vitapelekwa kwenye hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya
matibabu ya watoto hao. Alisema kuwa, mbio za kilometa 10 na 21 zitatumika zaidi kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na umuhimu wa bima. “Tunajisikia fahari kudhamini mashindano haya kwa ajili ya kusaidia jamii. Tunaomba wadau washiriki ili kufanikisha lengo au kuzidi lengo hilo. Naomba pia nitoe rai kwa jamii nzima aidha kushiriki mbio hizi au
kuwasajili ndugu na marafiki ili tuweze kuwagusa watoto wengi zaidi wenye saratani kupata matibabu hospitali
ya Muhimbili,” alisema Mponzi.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *