Mbosso Akosa Mamilioni!

MWANAMUZIKI pendwa wa Bongo Fleva, Mbwana Yusuf Kilungi ‘Mbosso Khan’ anayetumikia Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), ameeleza namna alivyokosa mamilioni kutokana na shoo zake kufutwa.

 

Mbosso ameliambia Gazeti la IJUMAA WIKIENDA kuwa, alikosa mapato hayo kutokana na mlipuko wa janga la Virusi vya Corona ambapo nchi mbalimbali zilifunga mipaka yake na kusitisha mikusanyiko ya watu.

 

Mwimbaji huyo mkali amesema amejikuta akipotza shoo nyingi ambazo zingemuingizia kati ya shilingi milioni 80 hadi milioni 100 za Kitanzania.

 

“Nilikuwa na shoo ngingi sana kwa mwaka 2020. Nilikuwa hadi na shoo nchini Ufaransa. Shoo hizo zote nilitakiwa nizifanye kuaniza mwezi wa nne hadi sasa. Lakini naamini mambo yatakaa sawa tena,” amesema Mbosso ambaye pia ni mtunzi wa nyimbo nyingi na kubwa.

 

Kabla ya Mbosso kusema hivyo, bosi wake kwenye Lebo ya Wasafi, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alisema kwa upande wake amepoteza zaidi ya shilingi bilioni 3 kutokana na janga la Corona.

 

STORI: MWANDISHI WETU, DARToa comment