Mbunge Aliyenaswa Akifanya Ufusika na Mchepuko Bungeni Ajiuzulu

Mbunge wa Argentina, Juan Emilio Ameria amejiuzulu Ubunge ikiwa ni siku chache baada ya kusimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge kutokana na kunaswa akibusu maziwa ya mchepuko wake wakati kikao cha Bunge kikiendelea (LIVE) kwa njia ya mtandao.

 

Mbunge huyo ambaye ameoa na ana watoto watatu alikuwa akijivinjari na Mchepuko wake wakati vikao vya Bunge vikiendelea online kutokana na corona ambapo ghafla Mpenzi wake alimkalia mapajani na wakaingia mahabani.

 

“Nimejisikia vibaya sana, nilihisi kwamba nimelog out na kuondoka kwenye kikao kwa muda kumbe nilikuwa bado hewani, Wabunge wenzangu wote wameona tukio na kibaya zaidi video imerekodiwa na kusambazwa, naiomba radhi Familia yangu,” – Juan.
Toa comment