Mbwa watumika kubaini wenye CORONA uwanja wa ndege Finland (+Video)

2 0

Mbwa wa kunusa waliopewa mafunzo ya kubaini Covid-19 wamepelekwa uwanja wa ndege wa Finland Helsinki-Vantaa kusaidia kukabiliana na janga la corona.

Majaribio yanafanyiwa abiria waliojitolea. Mtafiti anayeongoza utafiti huo anasema majaribio hayo yameonesha matokeo ya kufana lakini usahihi wa mbwa hao bado haujathibitishwa.

”Nchini Finland, kuna mradi wa unaowahusisha mbwa kunusaabiria katika uwanja wa ndege wa Finland Helsinki-Vantaa wanaojitolea.”- Kwa mujibu wa taarifa za utafiti

”Watu wanafutwa shingoni kwa vitambaa, kisha sampuli hiyo hupewa mbwa aliyefunzwa kunusa na akibweka inamaana virusi vimebainika. Matokeo yake yanawasilishwa kwa dakika.”

 

IMEANDIKWA NA @fumo255 (Video Creadit by Guardian News)

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *