Mdee: Gwajima Kitu Gani? Tutakutana Jukwaani

HALIMA Mdee, Mgombea Ubunge Kawe, Dar es Salaam kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amesema ‘Gwajima (Josephat Gwajima) kitu gani.’ Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam.

 

Amesema, kwenye uchaguzi mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020, katika Jimbo la Kawe alilokuwa akiliongoza kwa miaka kumi mfululizo, mshindi atatokana na mkakati wake kwa wapiga kura.

 

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne tarehe 25 Agosti 2020, muda mfupi baada ya kurudisha fomu ya uteuzi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kugombea jimbo hilo na kukidhi masharti ya ujazaji wa fomu ya uteuzi.

 

Akimjibu mwandishi baada ya kuulizwa maandalizi yake ya kukabiliana na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Gwajima, mgombea wa CCM kwenye jimbo hilo amesema “Gwajima? Sina muda wa kujadili wagombea wenzangu, tukutane field (uwanjani). Kila mtu atashinda kwa mziki wake,” amesema Mdee.

 

Hata hivyo, amesema, zoezi la urudishaji fomu kwa upande wake halikuwa na changamoto yoyote kwani fomu yake imepokelewa.Toa comment