Meya Iringa Aliyevuliwa Cheyo Chake Akabidhi Ofisi

ALIYEKUWA Meya wa Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe leo Jumanne, Machi 31, 2020, amekabidhi ofisi yake pamoja na gari aliokuwa akitumia kwa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Himid Njovu baada ya kukamilisha taratibu za kiofisi.

 

Kimbe aliondolewa madarakani kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka, na rasilimali za halmashauri hiyo katika shughuli binafsi.

 

“Baada ya kupata mukhtasari nikafikiria kwamba hata nikisema niendelee kubaki madarakani kitakachofanyika maana yake Mkurugenzi hata itisha vikao kwa hiyo nimeona ni busara kuwahurumia wananchii wa Iringa na nikabidhi ofisi ili niruhusu vikao vya halmashauri kufanyika,” amesema Kimbe.
Toa comment