Mfahamu mshambuliaji hatari wa miaka 53, King Kazu

3 0

Mshambuliaji wa klabu ya Yokohama FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Japan maarufu kama ‘J-League’, Kazuyoshi Miura amekuwa mchezaji wa kwanza mwenye umri mkubwa wa miaka 53 kusakata kabumbu.

Nahodha huyo wa Yokohama FC, Kazuyoshi Miura akiwa na umri wa miaka 53 hapo jana ameshindwa kukitetea kikosi chake na kujikuta kikiambulia kipigo cha jumla ya magoli 3 -2 mbele ya vinara wa Ligi hiyo timu ya Kawasaki Frontale mchezo uliyopigwa kwenye dimba la Kawasaki Todoroki.

Kazuyoshi Miura became the oldest player to appear in the Japanese top flight aged 53

Kazuyoshi Miura maarufu kama ‘King Kazu’, alianzia soka lake nchini Brazil mwaka 1986 kwasababu kipindi hicho  Japan hakukuwa na profeshino Ligi ambayo ingemfanya yeye kutimiza ndoto zake za kucheza soka, licha kuvalia kitambaa cha unahodha hapo jana alishindwa muwahamasisha kikosi chake ili kutoka na pointi tatu uwanjani.

“Nilipoingia uwanjani, nilikuwa na hisia kubwa mno ya kutimiza wajibu wangu na kuwafanya kila mmoja pale ndani kuwa kwenye hisia moja,” Miura alinukuliwa akisema na shirika la habari la Kyodo.

Hiyo ilikuwa ni mechi yake ya kwanza ‘King Kazu’ kucheze ya katika Ligi kuu nchini Japan tangu mwaka 2007. Klabu  ya Yokohama ilikuwa ikicheza ligi daraja la pili kwa miaka 12 kabla ya kufanikiwa kupanda daraja msimu uliyopita.

Miura amefanikiwa kufunga jumla ya magoli 55 kwenye michezo 89 aliyocheza nchini Japan wakati mchezo wake wa miwisho na timu yake ya taifa ilikuwa mwaka 2000 na kufanikiwa kuvunja rekodi ya mshambuliaji, Masashi Nakayama ambaye alikuwa anacheza akiwa na umri wa miaka 45 akiwa na timu ya Consadole Sapporo mwaka 2012.

‘King Kazu’ siyo veterani pekee aliyekuwa kwenye mchezo huo wa hapo jana siku ya Jumatano, lakini pia aliyekuwa kiungo wazamani wa Japan na Celtic, Shunsuke Nakamura mwenye umri wa miaka 42 pia alikuwa sehemu ya kikosi cha Yokohama kilichoanza.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *