Mgombea Urais Adaiwa Kuondoka Nchini – Video

6 0Mgombea Urais Adaiwa Kuondoka Nchini – Video

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amedai kuwa mmoja wa wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia moja ya chama pinzani (bila kumtaja jina) ameondoka nchini baada ya kuona ‘amezidiwa mapigo’ na kampeni za CCM.

 

Polepole amesema hayo leo Ijumaa, Septemba 11, 2020 wakati akizungumza na wanahabari mkoani Geita na kutoa tathmini ya kampeni za CCM kwa siku 12 walizofanya na kutoa mwongozo kwa awamu ya pili ya kampeni za chama hicho.

 

“Kampeni kwa ujumla inakwenda vizuri sana, tumewafikia Watanzania na wametuelea mno, tumefanya tafiti za Kisayansi kwa sababu tupo makini, kama kura zikipigwa sasa hizi Mhe. Magufuli anaibuka na ushindi mnono wa asilimia 85, sasa hivi tunajazia tu kura.

 

“Kwa mujibu wa Kitengo chetu cha taarifa cha chama chetu, kule mambo yameharibika, tumeona mmoja wa wagombea amekimbia, amechomoka mapema sana usiku wa kuamkia leo, hayupo nchini hapa, tena kuna dalili za kusindikizwa na ubeberu.

 

“Huyu jamaa amekwenda Dubai juzi alihudumu mambo ya nje kule, ndiyo walikuwa wanakutana angani atatueleza nini yule?

 

“Mzee Jakaya Kikwete yupo Ukanda wa Kusini kule anavuruga, Mzee Pinda na Spika Job Ndugai nao wanaendelea. Muziki ni mzito mpaka sasa tunapozungumza kuna mgombea mmoja amekimbia yupo nje ya nchi, ameona maji yamemfika shingoni, tunafanya kampenzi za kisayansi.

 

Polepole amesema kampeni za CCM 2020 zinafanyika kisayansi, kwani viongozi waandamizi wa chama hicpo wapo maeneo tofauti huku msafara mkuu ukiongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli, msafara mwingine unaongozwa na mgombea mwenza wa urais, Mhe. Samia Suluhu, na mwingine unaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Kuu ya CCM, Kassim Majaliwa.

 

“Tazama Ilani zao, mtu makini anaweza kusema mkinipa nchi nitawaletea ubwabwa? Mwingine anasema ‘Kazi na Bata’, dini gani inaruhusu starehe, imeandikwa ‘Utafanya kazi, kwa jasho lako utakula’, kuna bata hapo? Mwingine ‘Uhuru Haki Maendeleo’ hii sio kaulimbiu,” amesema Polepole.

 Toa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *