Mke wa Rayvanny Abanwa Kumkuwadia Mondi

24 0

Mke wa Rayvanny Abanwa Kumkuwadia Mondi

UKISIKIA mambo ni moto ndiyo haya sasa! Wakati mwandani wa mwanamuziki wa kimataifa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna akiwa leba akijifungua hivi karibuni, uliibuka ubuyu matata kuwa jamaa huyo anachepuka.

FAHYMA MFANIKISHAJI

 

Huku na huku ikaelezwa kwamba facilitator (mfanikishaji) wa ishu hiyo ni mke wa staa wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ ambaye Diamond ni bosi wake pale Wasafi, Fahyma ‘Fayvanny’ ambaye alikuwa akimkuwadia mwanamitindo Hamisa Mobeto kwa Diamond au Mondi. Mambo yakawa ni mengi na mji ukawa mzito kuwa, Fahyma ni rafiki mkubwa wa Hamisa hivyo alitaka kumrejesha kwa Mondi ambaye alishakuwa naye zamani na wakafanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume, Dyllan.

 

TANASHA  ALIPONYAKA ISHU

Kwa upande wake, Tanasha wakati akifurahia kupata mtoto wa kiume na Mondi huku akisota leba pale Hospitali ya Aga Khan jijini Dar kwa saa takriban 17, alipotoka hospitalini akafikishiwa ishu na kumsababisha kucharuka kinoma. Kwa mujibu wa chanzo makini cha gazeti hili, zilipita siku kadhaa, Tanasha na Mondi wakawa hawaelewani kama mwanzo kwa sababu ya meseji za kimapenzi zilizodaiwa kunaswa.

 

Ilidaiwa meseji alizonasa Tanasha kwenye simu ya Mondi zilikuwa zinatoka kwa Hamisa. “Kiukweli mapenzi ya Mondi yaliyumba mno kiasi cha kupumulia mashine. “Watu walikuwa wanamuonea huruma yule binti wa watu kutokana na mambo yaliyokuwa yanamtokea huku akiwa ndiyo kwanza ametoka kujifungua.

MONDI NA HAMISA TENA?

“Ishu kubwa ilikuwa inasemekana eti jamaa (Mondi) alikuwa anataka kurudisha majeshi kwa Hamisa, hivyo wakawa wanatumiana meseji na chating huku wakiahidiana kuoana. “Hata hivyo, hadi mwisho wa sakata hilo haikujulikana mara moja kama wamekubaliana kuoana au la. “Kwa kifupi, meseji na chating za Mondi na Hamisa ndizo zilileta balaa.

 

“Baada ya kuona maji yamekorogeka, ilibidi Tanasha amuombe Fahyma, akaongee na Hamisa ili amuachie mume wake bila kujua huyo Fahyma ndiye connector (muunganishaji). “Unaambiwa watu wanaoijua ishu kamili, ndiyo wakambana Fahyma kila kona huku wakimtaka kuacha dhambi ya usaliti kwa mtoto wa watu.

FAHYMA ABANWA

“Kwa hiyo ninyi kama mnataka ubuyu kamili mpigieni Fahyma mumuulize ukweli, maana nasikia alibanwa hadi kijasho chembamba kikamtoka na sijui kama ana ukaribu tena na Tanasha kama mwanzo,” kiliweka nukta chanzo chetu kwa sharti la kutotajwa jina hadi masia atakaporudi.

 

MSIKIE FAHYMA

Gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Fahyma na baada ya kupatikana alisema kuwa, hata kama ni kweli yeye hawezi kueleza jambo lolote. “Unajua mimi siyo pikipiki Posta eeh? Halafu Diamond na Tanasha wanapendana jamani, hata kama wana matatizo ni yao wawili, mimi hawawezi kunitumia kama kipikipiki Posta kwa Hamisa.

 

“Kwanza, Tanasha hawezi kunituma, na mimi kufanya hivyo ni kitu ambacho hakiwezekani japokuwa ni kweli wote (Tanasha na Hamisa) ni rafiki zangu na mara nyingi nimekuwa nao sehemu mbalimbali. “Lakini siwezi kuwa kuwadi wa mapenzi yao, nitakuwa nakosea sana. “Kwa kifupi tu ni kwamba, Diamond na Tanasha hata kama wana matatizo, wanayamaliza wenyewe,” alisema fahyma ambaye kuna madai kuwa alifunga ndoa ya kimyakimya na Rayvanny.

TANASHA ANASEMAJE?

Katika maelezo yake juu ya ishu hiyo alipohojiwa, Tanasha hakupenda kuongea sana zaidi ya kusema tu kwa kifupi kwamba anamuamini mzazi mwenzake hivyo wanaojibebisha kwake waache mara moja. “Sijali kuhusu uhusiano wake uliopita, ninaangalia nilipo sasa. “Ninamuamini sana Diamond, kwa hiyo naomba hao wanaomfuatilia waache,” alisema Tanasha.

STORI: Memorise Richard, Risasi Jumamosi

Toa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *