Mkuu wa UN ayataka mataifa tajiri kuacha kutegemea makaa ya Mawe na mafuta 

1 0

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameitaka Japan na mataifa mengine tajiri kuachana na kutegemea makaa ya mawe na mafuta mengine ya kuchimbwa ardhini na kuwekeza katika vyanzo vya nishati salama wakati mataifa hayo yanajitoa kutoka janga la virusi vya corona.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito huo katika hotuba kwenye mkutano kwa njia ya vidio uliofanyika nchini Japan. Guterres amedokeza kuwa nchi nyingi zinatumia fursa ya janga kuongeza matumizi ya nishati salama pamoja na juhudi nyingine, zenye lengo la kufikiwa kwa lengo la kupunguza ongezeko la ujoto duniani hadi nyuzi joto 1.5.

Mkutano mkuu wa Umoja wa mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi unaotarajiwa kufanyika mjini Glasgow, Scotland, mwezi Novemba umeahirishwa kutokana na janga la virusi vya corona. Ukifahamika kama COP 29 mkutano huo utafanyika mapema mwezi Novemba mwaka 2021.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *