Mkwasa Kukabidhiwa Mikoba Ya Mbelgiji

MABOSI wa Klabu ya Yanga wamechungulia mbali na kuona ligi inaweza kurejea hivi karibuni lakini bila ya kuwa na makocha wao wawili, Kocha Mkuu Luc Eymael na yule wa viungo, Riedoh Berdien raia wa Afrika Kusini.

 

Sasa kwa ajili ya kuweka mipango sawa bila ya kutetereka, mabosi hao wa Yanga wameamua kumuachia mikoba kocha msaidizi, Charles Mkwasa kuwa ndiye awe msimamizi mkuu wa timu hiyo wakati ambao Eymael atachelewa kurejea nchini endapo tangazo la ligi kuendelea litakapotangazwa.

Mabosi hao wamefi kia muafaka huo baada ya kuona Eymael ni ngumu kurejea Bongo kwa sasa kutokana na kwao, Ubelgiji kufunga uwanja wa ndege kutokana na janga la Corona ambapo pia akirejea atatakiwa kubakia karantini kwa siku 14.

 

Habari ambazo Championi Ijumaa limezipata ni kwamba timu hiyo itakuwa chini ya Mkwasa ambaye wamejiridhisha kuwa kutokana na uzoefu wake, ataweza kuibeba timu hiyo kwenye mechi zilizobaki.Kabla ya kuja Eymael, Mkwasa aliachiwa timu hiyo baada ya kocha mkuu Mwinyi Zahera kuvunjiwa mkataba wake.

 

“Inaonekana labda kocha Eymael anaweza kuchelewa kurejea Bongo kama ligi itaanza hivi karibuni, lakini hilo tayari limeshafanyiwa utaratibu wa kuweza kulikamilisha na kuwa vizuri.

 

“Kitakachofanyika ni kuwa Mkwasa ndiye atapewa timu aiendeshe kwa wakati huo kwa sababu wengi wamemuamini kutokana na kile alichokifanya wakati alipopewa timu baada ya Zahera kuvunjiwa mkataba,” kilisema chanzo hicho.Kwa upande wake, Ofi sa Mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz, amesema mipango hiyo wanaendelea nayo kuhakikisha hawapati tatizo lolote hata kama kocha huyo atachelewa kurudi na ligi ikianza.

Stori: Said Ally, Dar es SalaamToa comment