Mmoja auawa na wengine wajeruhiwa vibaya katika shambulio la kuchomwa visu, Uingereza

1 0

Polisi nchini Uingereza imesema kuwa mtu mmoja ameuawa na wengine saba wamejeruhiwa kwa kisu katikati tukio lililofanyika katika jiji la Birmingham.

Tukio hilo halijaonekana kuhusishwa na ugaidi, genge la kihalifu au kuhusishwa na machafuko yoyote Polisi wa West Midlands wamesema.

Hata hivyo uchunguzi dhidi ya mtu aliyohusika na tukio hilo unaendelea huku polisi wakiwataka wenye CCTV, au klipi ya video kupitia simu waziwasilisha ili kusaidia kufanikisha kwa zoezi hilo.

Kwenye tukio hilo mwanaume mmoja amepoteza maisha huku wengine wakiwa wamejeruhiwa vibaya.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *