Mobeto Amponza Dimpoz – Global Publishers

20 0

 Mobeto Amponza Dimpoz

WANANZENGO siyo watu wazuri! Ile tabia ya staa wa Bongo Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ kuwanyapianyapia warembo ambao walibanjuka penzini na staa mwenzake wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ imemtokea puani baada ya kugusa anga za mwanamitindo Hamisa Mobeto.

 

Iko hivi; kwenye moja ya mahojiano aliyoyafanya Dimpoz hivi karibuni, alisema anamhusudu mno Mobeto kwani ni mrembo mwenye kila sifa ya yeye kumuoa.

Kama hiyo haitoshi, Dimpoz alikwenda mbali zaidi baada ya kuposti kipande cha video cha Mobeto katika ukurasa wake wa Instagram na kusindikiza na ujumbe wa kumsifia uliosomeka hivi;

 

“Sasa tujadili wimbo au tujadili hiki KISHINGO AMAIZING?…”

Baada ya kuandika ujumbe huo, Mobeto alimjibu; ‘VYOTEE’, jambo ambalo liliamsha hisia kwa mashabiki wa Diamond au Mondi ambao hawakupenda ampe ushirikiano.

Hapo ndipo mashambulizi yalipoanza kuporomoshwa kwa Dimpoz ambapo walimsema kuwa anapoteza mvuto kwa kumfuatafuata mrembo huyo aliyewahi kutembea na msanii wao, Diamond.

Mashabiki hao walizidi kumuandama Dimpoz kwa kufukua ‘makaburi’ ambapo walirudi nyuma na kukumbusha orodha ya warembo ambao Diamond aliwaacha, halafu yeye ‘akaruka’ nao.

 

“Huyu jamaa sijui vipi, kwa Wema ilikuwa hivihivi hadi akasababisha ugomvi mkubwa sana wa kutukanana na Diamond, lakini pia kwa Zari (Zarinah Hassan) nako akajipitisha, sijui yupoje huyu,” alichangia jamaa aliyejiita Kitos Instagram.

Gazeti la Ijumaa Wikienda lilimvutia waya Dimpoz kuhusiana na ishu hiyo, lakini simu yake iliita bila kupokelewa.

 

Hata hivyo, kwenye ukurasa wake wa Instagram, shabiki mwingine alimsifia Dimpoz kwa kuwa karibu na mrembo huyo na kumshauri amkutanishe na Zari.

“Dimpoz ungewapatanisha Zari na Mobeto wakawa marafiki bora, upande wa pili wangetamani kulia,” alichangia Anita Instagram.

 

Dimpoz na Mondi ambao walikuwa marafiki wa damu, walitofautiana miaka kadhaa iliyopita na kufikia hatua ya kutukanana matusi ya nguoni ambapo bifu lao limeendelea kudumu chinichini hadi leo.

Ugomvi wao huo ulihusishwa na masuala ya wapenzi japo wenyewe hawakuanika kiini hasa cha ugomvi wao.

Toa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *