Mobeto, Tajiri Mambo Moto!

UTAKE, usitake utasemwa tu; hata ukijifukia chini! Ndivyo ilivyo kwa mwanamitindo na mjasiriamali hapa Bongo, Hamisa Mobeto ambaye kwa sasa anasemwa kutoka kimapenzi na bwa’mdogo tajiri wa mtaani, Fred Vunjabei.

 

Mobeto amekuwa hataki maneno na mtu kwa maelezo kuwa amejikita zaidi kwenye kusaka pesa, lakini mambo kati yake na Vunjabei yamekuwa moto. Kwenye mitandao ya kijamii kelele za wawili hao kuwa kapo mpya tauni zimekuwa nyingi huku mapichapicha yakitengezwa kuwa mwanamitindo huyo anawezeshwa kimaisha na Vunjabei.

“Jamaa kafi ka, kampangia bishosti nyumba na kamnunulia gari la kifahari,” nyepesi za mtandaoni zilisambazwa kila kona na kuambatana na komenti kibao. Kwa kuwa mambo ya wawili hao yamekuwa moto waandishi wetu wakaona mambo yasiwe mengi, Mobeto atafutwe ili afunguke juu ya madai hayo.

 

Akipiga stori juzi kati na Amani kuhusiana na ishu Hamisa amesema wao ni washikaji tu, la kustaajabisha hakuna. “Sijui kwa nini watu wanaongea maneno kama hayo, Fred ni mshikaji wangu, ni kama kaka yangu.

“Kingine, ukaribu wetu unaowafanya watu waongee unatokana na biashara, mimi ni mfanyabiashara na yeye ni mfanyabiashara hivyo huwa tunashirikiana kwenye masuala ya biashara tu.

“Watu wanatakiwa wajue kwa sasa niko busy na biashara zangu na siangalii mambo mengine yasiyokuwa na maendeleo ndiyo maana muda mwingi nashinda dukani kwangu,’’ alisema Hamisa.

Ukaribu wa Hamisa na Vunjabei uliingiwa na mashaka kiasi cha watu kuwajadili hasa baada ya Mobeto kuonekana mkoani Iringa ambako Vunjabei alikuwepo na kushirikiana na wasanii wengine kufungua duka lake mkoani humo.

 

Basi kwa kuwa Mobeto kasema yake ngoja tuamini nukta hiyo huku tukiendelea kumsaka Vunjabei ambaye hakupatikana ili kubalansi stori yetu. Endapo naye akisema hakuna mapenzi kati yao ukurasa utafungwa rasmi na kuwafanya wajadili ya wenzao wachukue jembe wakalime.

 Toa comment