Mondi Kuvuna Mamilioni Mbele ya Rick Ross na Chris Brown

1 0Mondi Kuvuna Mamilioni Mbele ya Rick Ross na Chris Brown

SUPASTAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anatarajia kuvuna mamilioni kama yote katika shoo maarufu kwa jina la AfroNation. Kwenye shoo hiyo inayotarajia kufanyika Julai 2021 nchini Ureno, Diamond au Mondi, atashea jukwaa moja na mastaa wakubwa duniani, akiwemo Rick Ross na Chris Brown kutoka Marekani.

 

Tamasha hilo ambalo limepangwa kufanyika kwa muda wa siku tatu, kuanzia Julai 1 mpaka 3, litahudhuriwa na mastaa mbalimbali kama Sauti Sol toka nchini Kenya, Burna Boy, Davido, Flavour, Olamide, Patoranking, Reekado Banks, Tekno, Yemi Alade na Wiz Kid.

 

RISASI

lilizungumza na mtu wa karibu na lebo ya Wasafi Classic Baby ‘WCB’ inayomilikiwa na Mondi, ambapo bila hiyana, aliweka wazi kuwa mkali huyo ataenda kuvuna mamilioni ya fedha, kwani shoo zake zote za nje, huwa zinaanzia shilingi milioni 100 na kuendelea.

 

“Kwanza tumefurahi sana Mondi kuwa mmoja wa wasanii Afrika, ambao wamechaguliwa kwenda kupafomu siku hiyo, hivyo watu wajue tu kwamba kupitia shoo hiyo, atavuna mpunga mrefu sana.

 

Nyie wenyewe si mnajua Chibu hafanyi shoo chini ya milioni 100, sasa wewe fikiria anaenda Ureno, unadhani watamlipa kiasi gani?

Tunaomba tu mashabiki waendelee kumsapoti ili naye aendelee kuongeza juhudi ya kufanya vizuri zaidi,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa jina.

 

MENEJA ANASEMAJE?

RISASI lilimvutia waya meneja wa Mondi, Said Fella ‘Mkubwa Fella’ ili kutaka kujua idadi kamili ya pesa atakayopata msanii wake kwenye shoo hiyo, ambapo baada ya kupokea, aliomba atafutwe meneja mwenzake kwa kuwa yupo bize na masuala ya siasa.

 

“Nikiongea hapa nitakudanganya, kwa sababu sijafuatilia kabisa hiyo ishu, nipo bize na kampeni, lakini unaweza kumcheki Sallam, yeye ndiyo ana majibu kamili,” alisema Fella. Hata hivyo, mwandishi wetu alimpigia Sallam Shariff ‘SK’, ambapo simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

STORI: MEMORISE RICHARD, RISASI JUMAMOSI

 Toa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *