MORRISON NISIKIO LA KUFA – Gazeti la Dimba

27 0


NA JESSCA NANGAWE

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Benard Morrison, ameendelea kukumbwa na matukio ya utovu wa nidhamu ndani ya kikosi chake kwa siku za hivi karibuni.

Wakati sakata lake la kushindwa kusafiri na timu likiwa bado la moto, kiungo huyo anadaiwa kutoroka kambini bila ruhusa ya viongozi wake wakati timu ikijiandaa na mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Kagera Sugar uliopigwa jana Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa Morrison raia wa Ghana aliyejiunga na Wanajangwani hao kwenye usajili wa dirisha dogo mwaka huu, alizuiwa kuondoka kambini hapo na walinzi ambao waligundua njama zake, lakini aliwazidi nguvu na kutoroka.

Mmoja wa wachezaji ndani ya timu hiyo ambaye hakutaka jina lake litajwe aliliambia DIMBA Jumatano kuwa ni kweli mchezaji huyo aliondoka kambini hapo na haikufahamika mara moja ni wapi alipoelekea. “Sifahamu lakini ninachojua kwasasa hayupo kambini, siwezi kusema lolote kuhusu yeye,” alisema mchezaji huyo.

Tukio hilo linaendelea kuwa mfululizo wa matukio ya utovu wa nidhamu yanayomkabili mchezaji huyo huku ikidaiwa yupo mbioni kutimkia moja ya klabu nchini Kuwait. Kwa upande wa viongozi wake, wamedai kwasasa hawawezi kuzungumzia lolote kuhusu mchezaji huyo na akili yao wanaielekeza katika michezo yao ya Kombe la FA inayoendeleaSource link

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *