Mourinho kumrudisha Costa England, je unakumbuka kitu gani kwa wawili hawa?

6 0

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kuwa Kocha wa Tottenham, Jose Mourinho amepewa nafasi ya kuungana tena na striker wake wa zamani wa Chelsea,  Diego Costa kama atahitaji kufanya hivyo.

Mourinho ambaye ni raia wa Ureno amekuwa akifanya usajili kipindi hiki ili kukiboresha kikosi chake kujiandaa na msimu mpya wa 2020-21 wakati tayari amewashusha kiungo Pierre-Emile Hojbjerg na goli kipa Joe Hart.

Mourinho akiwa katika harakati za kumsajili nyota wa klabu ya Welves, Matt Doherty amepatiwa ofa ya kumsaji mshambuliaji Costa kutoka Atletico Madrid.

Atletico Madrid are open to selling the former Chelsea forward, according to reports

Tottenham imekuwa ikimtegemea sana Harry Kane katika safu yake ya ushambuliaji na hivyo kama inahitaji kuongeza ubora wake katika nafasi hiyo italazimika kumsajili Costa.

Mourinho na Costa wamewahi kufanya kazi pamoja pale darajani, Stamford Bridge hvyo ni watu ambao wanafahamiana vema.

Mourinho and Costa worked together at Stamford Bridge for one year and won a league title

Mhispania huyo amekuwa akihaha kurudi katika kiwango chake baada ya msimu uliyopita kufunga magoli matano pekee kwenye michezo 30 aliyocheza Atletico.

Ingawa Costa amesalia na mwaka mmoja katika mkataba wake, Atletico wapo tayari kumuuza kuliko wamuache aonde bure ifikapo mwakani 2021.

Tottenham wataanza mbio za kusaka ubingwa wa Premier League msimu mpya kwa kukabiliana na Everton wakiwa nyumbani Septemba 12.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *