Msondo Ilivyokiwasha Mbagala Usiku Wa Kuamkia Leo

1 0Msondo Ilivyokiwasha Mbagala Usiku Wa Kuamkia Leo

Bendi kongwe isiyochuja Msondo Music usiku wa kuamkia leo kama kawaida yake ilikiwasha ndani ya Ukumbi wa Baa ya Kisuma iliyopo Mbagala Sabasaba Dar.

Onesho hilo lilifurika mashabiki kindakindaki wa bendi hiyo ambapo walionesha hisia zao kwa kuserebuka mwanzo mwisho.

Makamuzi hayo yalifanywa na mastaa wa bendi hiyo, Karama Regesu, Ridhiwani Pangamawe, Hassani Moshi a.k.a TX Junior, Roman Mng’ande ‘Romario’ Rijo Voice, Juma Katundu, Eddo Sanga, Davido Bass na wengineo ambapo Mzee Said Mabera ndiye aliyekosekana.

Mashabiki wa bendi hii ni wanadaiwa kuwa ni wa ajabu sana ambapo inasemekana kuwa eti uwepo tu wa mastaa hao mbele ya macho yao ni tayari ni burudani tosha hata wasipopanda jukwaani kuimba wala kupiga chombo chochote.

Angalia shoo nzima ilivyokuwa.

Eddo Sanga (kushoto) na Juma Katundu wakifanya mambo.                                                                                 

Mshindi wa Tuzo ya Kill ya Mtunzi Bora miaka kadhaa iliyopita Karama Regesu (kushoto) akiwajibika.                                                                                                                                                                                   

Hassan Moshi a.k.a TX Junior akipelekana mdogomdogo na shabiki.

Sehemu ya mashabiki waliofurika kwenye onesho hilo.

Romario akimchagiza mmoja wa mashabiki aliyekuwa akizunguusha nyonga.

Karama Regesu na Romario wakitoa shoo kali ya mbwembwe na machejo mbele ya mashabiki.

Shabiki akicheza kwa hisia kali alipokunwa na moja ya ngoma zilizokuwa zikipigwa.

HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPLToa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *