Mtandoa wa TikTok uko mbioni kuondoa video ya mtu aliyekuwa akijitoa uhai

4 0

Matandao wa kijamii wa TikTok unajitahidi kuondoa kanda ya video inayomuonesha mtu akijjitoa uhai. Video hiyo ambayo imekuwa ikisambazwa kwenye mtandao huo kwa siku kadhaa, ilianzia kwenye Facebook na sasa imeanzakusambazwa Twitter na Instagram.

M

TikTok ni maarufu kwa vijana wadogo – na baadhi yao wameripotiwa kutazama video hiyo na wamepata usumbufu wa kimwazo.

Mtandao huo umesema utawapiga marufuku akaunti za watu watakaoendelea kusambaza video hiyo mara kadhaa.

”Tunawashukuru wafuatiliaji wa mtandao wetu ambao wameripoti kuhusu video hiyo na kuwatahadharisha wengine dhidi ya kuitazama ama kushirikisha maudhui kama hayo kwenye jukwaa lolote, kwa heshima ya mtu huyo na familia yake” mwakilishi wa TikTok alisema.

Kwa upande wake Facebook imeiambia BBC: “Tulifuta video hiyo mwezi uliopita kwenye mtandao Facebook, siku iliyooneshwa moja kwa moja, na kutumia mfumowa teknolojia kufuta nakala za video zinazochapishwa kutoka wakati.

“Tunatoa pole zetu kwa familia ya Ronnie na marafiki wakati huu mgumu.”

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *