Mtangazaji wa ITV, Agnes Almasy aagwa rasmi Dar Es Salaam na kwenda kuzikwa Tanga (+Video)

8 0

Mtangazaji huyo alipatwa na umauti  Septemba 3 Buguruni Jijini Dar es Salaam alipokuwa akijiandaa kuelekea kazini na alifariki akiwa njiani kuelekea hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam.

Misa hiyo ya kuaga ilihudhuriwa na viongozi wa IPP Media, wafanyakazi na watu mbalimbali wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One Joyce Mhaville.

Agnes alikuwa mchapakazi mzuri sana, aliyependa kujifunza kila siku na alikuwa mchangamfu sana na mwenye kupenda kufurahi muda mwingi kwakweli tumepoteza mfanyakazi mahiri na aliyefanya kazi zake kwa ufanisi mkubwa“, amesema Julieth Robert ambaye ni Mfanyakazi na msomaji habari wa ITV.

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa ajili ya maisha ya Agnes Almasy kwani sote tulitoka kwa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea”, ameongeza.

Baada ya Ibada ya kuaga mwili, marehemu anatarajiwa kusafirishwa kuelekea Mkoani Tanga ambapo atazikwa katika Makaburi ya Bombo.  Agnesy ameacha mume na mtoto mmoja na aliajiiriwa rasmi kufanya kazi na ITV na Redio One Machi 19, 2018.

 

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *