Muangola Wa Yanga Aanza Kazi Rasmi

KIUNGO mpya wa Yanga, Carlos Stenio Fernandez Guimaraes ‘Carlinhos’ baada ya kutua jana rasmi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,(JNIA) na kumalizana na mabosi wa Yanga, leo Agosti 26 ameanza mazoezi na wachezaji wenzake.

 

Yanga ilianza mazoezi Agosti 10, Uwanja wa Chuo cha Sheria ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu Bara ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 6.

Mchezo wa kwanza kwa Yanga itakuwa dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Mkapa, Septemba 6.

Akiwa mazoezini ameonekana akiwa ni mwenye furaha huku akikaribishwa na wachezaji wenzake ambao tayari walishaanza mazoezi kwa kuimba naye na kucheza ikiwa ni pamoja na Tuisila Kisinda, Tonombe Mukoko.

Kiungo huyo aliyepokelewa na mamia ya mashabiki wa Yanga jana, Agosti 25 alipokuwa akitokea nchini Angola majira ya saa 7:20 amesema kuwa anafurahi kuwa ndani ya Yanga na anaahidi kufanya kazi zaidi kwa vitendo.Toa comment