Mugalu Arejea Fasta Dar

MSHAMBULIAJI mpya wa Simba, Mkongomani, Chris Mugalu, juzi alirejea nchini akitokea nyumbani kwao DR Congo alipokwenda kumaliza matatizo ya kifamilia.Mugalu ni kati ya wachezaji wapya wa kimataifa waliosajiliwa na Simba katika kukiimarisha kikosi hicho.

 

Wengine Larry Bwalya, Bernard Morrison na Joash Onyango.Mshambuliaji huyo alijiunga na Simba kama mchezaji huru baada ya mkataba wake na Lusaka Dynamos inayoshiriki Ligi Kuu ya Zambia kumalizika.

Akizungum-za na Spoti Xtra, Kocha Mkuu wa Sim-ba, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck, amesema kuwa mshambuliaji huyo tayari ametua nchini baada ya kumaliza ruhusa ya wiki moja aliyoiomba kwa ajili ya kumaliza matatizo ya kifamilia.

 

“Mugalu amerejea nchini juzi, lakini hatakuwa sehemu ya kikosi chetu kitakachocheza dhidi ya Ihefu Jumapili hii, yeye yupo Dar akiisubiria timu itakaporejea.

 

“Mshambuliaji huyo aliomba ruhusa maalum ya kurejea nyumbani kwao kwa ajili ya kumaliza matatizo ya kifamilia ambayo tayari ameyamaliza,” alisema Sven.Toa comment