Mume na Mke mbaroni kwa kusambaza taarifa za uongo kuhusu Corona “Serikali haina fedha wamefunga vyuo na shule kisingizio Corona” – Video

4 0

Jeshi la Polisi limewakamata wanandoa Boniface Elias Mwita (49) na Rosemary Elias Mwita (41) likiwatuhumu kusambaza taarifa za uongo kuhusu ugonjwa wa #COVID_19.


Wakiwa kwenye daladala wawili hao wamedaiwa kusema, “Serikali inapotosha Wananchi kwamba kuna virusi vya Ugonjwa wa Corona na pia Serikali haina pesa za kulisha wanafunzi ndio maana mashule na vyuo vimefungwa kwa kisingizio cha ugonjwa wa Corona, Pia Serikali ya Tanzania haina fedha kwa hiyo inataka msaada kutoka Mataifa ya nje’’.

 

“Polisi wanawashikilia watuhumiwa wawili Boniphace Mwita na Mkewe Rosemary wakazi wa Tabata,DSM kwa kusambaza taarifa za uongo kuhusu corona wakiwa kwenye daladala ambapo walianza kupotosha, kukejeli na kutania kwa kusema Serikali inapotosha Wananchi kwamba kuna corona”-Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum DSM

“Mwita na Mkewe tunawashikilia kwakuwa wakiwa kwenye daladala walisema Serikali haina fedha kwa ajili ya kulisha wanafunzi ndio maana mashule na vyuo vimefungwa kwa kisingizio cha corona na wakadai Serikali inafanya hivyo ili kuomba msada kwa Mataifa mbalimbali”

“Baada ya Mwita na Mkewe kusema Serikali inapotosha kuhusu corona na haina fedha ndio maana imefunga shule na vyuo kwa kisingizio cha corona, abiria ktk daladala iliwakera wakawaweka chini ya ulinzi wakamuamuru Dereva apeleke gari Polisi, tunao, tutawapeleka Mahakamani”

By Ally Juma.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *