Mume wa Shamimu Mwasha Asahau Neno la Siri Aomba Akabidhiwe CCTV Camera

Mfanyabiashara, Abdul Nsembo akitoka katika Mahakama Kuu Kitengo cha Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi hii leo.

Shamim Mwasha akiwa katika Mahakama Kuu Kitengo cha Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi hii leo.

 

Washtakiwa wawili ambao ni Mfanyabiashara, Abdul Nsembo na Mkewe Shamim Mwasha wanaokabiliwa na mashitaka ya kukutwa na dawa za kulevya wameshindwa kujitetea kutokana na kielelezo walichotarajia kukitumia kwa ajili ya utetezi kusahau neno la siri (password) hivyo akaomba wapatiwe vifaa hivyo kwa ajili ya kufuatilia paswed mpya.

 

Akiiambia mahakama mshtakiwa, Abdul Nsembo amedai kuwa angelitumia Ushahidi wa cctv kamera ambayo ilirekodi tukio lao wakati wanakamatwa, lakini amesahau paswed na hivyo akaomba mahakama imuruhusu apewe vifaa vya kielelezo hicho ili aweze kuwapatia watengenezaji kwa ajili ya kuweza kuifungua .

 

Baada ya kueleza hayo jaji anayesikiliza shauri hilo, Elieza Luvanda amesema kuwa maamuzi juu ya hoja yake atayatoa kesho kwamba wakabidhiwe vifaa hivyo au laa na kesi imeiahrisha hadi kesho saa tatu asubuhi.

 

Kesi hiyo kwa sasa ipo Mahakama Kuu Kitengo cha Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ambapo kwa Pamoja wanadaiwa Mei mosi mwaka 2019 walikutwa na dawa za kulevya nyumbani kwao maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.Toa comment