Musukuma: Shigongo Njoo Nikufundishe – Video

8 0Musukuma: Shigongo Njoo Nikufundishe – Video

MGOMBEA Ubunge wa Ji8mbo la Geita Vijijini, Mhe. Joseph Kasheku kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amemtaka Mgombea Ubunge wa Jimbo la Buchosa kupitia chama hicho, Eric Shigongo James kwenda kujifunza jimboni kwake namna ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ili kuwaletea maendeleo wananchi wake endapo atachaguliwa kuwa mbunge.

 

Msukuma amesema hayo leo Ijumaa, Septemba 25, 2020 wakati akihutubia kwenye uzinduzi wa kampeni za Shigongo katika viwanja vya Nyakaliro wilayani Buchosa.

 

“Ukienda jimbo la Geita Vijijini ninaloliongoza mimi yamewekwa mabango ya Rais tu, hakuna bango langu wala tisheti kwa sababu nilishamaliza uchaguzi, sio kwamba ninadharau digrii tayari Shigongo umesokma, unazo digrii, hakuna haja ya kusoma tena, badilisha Buchosa kwanza.

 

“Najua Mhe Rais alipokuja alituahidi kutengeneza lami kutoka Nkome mpaka Sengerema, lakini ukimaliza kampeni Shigopngo njoo ujifunze kwangu, kuna mabarabara ya vumbi lakini kama upo kwenye lami, tunataka mtu atoke Sengerama kuja hapa Buchosa anakimbia, huo uwezo tunao, sio haya mashimo ya barabara, Buchosa mmechagua mbunge mchapakazi.

“Mliniunganisha kwenye magrupu yenu ya WhatsApp bila kujua, nilikuwa naona mihemuko kwenye magrupu yenu, acheni makundi, acheni kubishana, nilikuja hapa 2015 kumnadi rafiki yangu Dkt. Tizeba, naijua Buchosa vizuri, kuna wavuvi kama ilivyo Geita Vijijini, tukitetea tunatetea pamoja.

 

“Tumekuwa tukizungumza mara nyingi unasema unataka uwe kama mimi, nakwambia una bahati sana kuwa na mwalimu Msukusma, tusimame pamoja kutetea watu wetu, kumtetea Rais wetu. Mhe. Rais anatoka kwetu, makaburi ya ndugu zake yapo hapa Katoma, anaijua Buchosa kila kitongoji, ndugu zangu msidanganywe, mchagueni Shigongo ana dhamira ya kweli ya kuwaleta maendeleo,” amesema Msukuma.

 
Toa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *