Mwalimu Mbaroni Kuishi Unyumba na Mwanafunzi

JESHI la Polisi Wilaya ya Igunga limemkamata mwalimu Keby Aron (32) kwa tuhuma ya kumweka kimada mwanafunzi wa miaka 17.

 

Mwalimu hiyo anayefundisha Shule ya Sekondari Nanga anatuhumiwa kuishi kwa zaidi ya miezi saba na mwanafunzi huyo anayesoma kidato cha tatu B katika shule hiyo.

 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Revocatus Kuuli, amethibitisha kuwa Polisi wamemkamata mwalimu  kwa tuhuma ya kufanya mapenzi na mwanafuzi.

 

“Ndugu zangu waandishi wa habari ofisa elimu sekondari hayupo yuko Tabora lakini kuhusu tuhuma ya mwalimu mimi kama mkurugenzi nimepata taarifa amekamatwa yuko Polisi hivyo mimi siwezi kulizungumzia zaidi suala hili tuviachie vyombo vya sheria,” alisema Kuuli.

 

Baba mzazi wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Joseph alisema mwanawe alikuwa anaishi na bibi yake (hakumtaja jina) kwenye kata ya Nanga.

 

Alisema bibi wa mtoto huyo alianza kuona tabia ya mjukuu wake ikibadilika hivyo akaanza kumfuatilia kwa karibu na ndipo alipobaini kwa mwanafunzi huyo anatembea na mwalimu Aron.

 

Joseph alisema, bibi huyo alimuuliza mjukuu wake kuhusu tabia yake na kwamba mwanafunzi huyo alimueleza kwamba amekuwa akifanya mapenzi na mwalimu huyo kwa muda mrefu.

 

Alisema, bibi huyo alimpigia simu baba wa msichana huyo anayeishi mkoa wa Mbeya na alipofika Igunga alikwenda kumshitaki kwenye vyombo vya dola na hatimaye mwalimu alikamatwa.

Chanzo: Habari LeoToa comment