Mwanafunzi: Sina Akili, Sitaki Shule, Bora Nifungwe Jela

MWANAFUNZI mwenye umri wa miaka 15 jina tunalihifadhi aliyefaulu kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza kwa wastani C katika matokeo ya darasa la saba mwaka huu wilaya ya Musoma mkoa wa Mara amegoma kwenda shule kwa kile anachodai hana akili ya kusoma masomo ya Sekondari.

 

Akizungumza akiwa nyumbani kwao mwanafunzi huyo amesema alifanya mtihani vibaya makusudi ili asiendelee kusoma lakini anashangaa kwanini amefaulu mtihani huo na kudai kuwa hayuko tayari kuendelea kusoma huku akiomba akajifunze kushona cherehani kwani anataka kuwa mwanamitindo.

 

Akisema hayo mbele ya Mkuu wa Wilaya, mwanafunzi huyo amesema yupo tayari kufungwa na sio kusoma.

 

Wazazi wa binti huyo wamesema wamesikitishwa sana na uamuzi wa mtoto wao na kudai kuwa binti yao ametoweka kusikojulikana tangu tarehe 25 mwaka jana na kumtafuta kila mahali lakini baada ya mkuu wa wilaya juzi kutangaza kuwakamata na kuwafunga wazazi ambao watoto wao hawajaripoti shule.

 

Baada ya kusikia hivyo, mwanafunzi huyo aliibuka na kuwataka wazazi wake wampeleke kwa mkuu wa wilaya ili akamueleze kuwa yeye binafsi hataki kusoma kama ni kufungwa afungwe jela yeye ila wazazi wake wasikamatwe na kufungwa jela.
Toa comment