Mwanaheri Na Siri Ya Mafanikio Kwenye Ndoa!

MUIGIZAJI mahiri wa filamu Bongo, Mwanaheri Ahmed amefunguka kuwa, aliamua kujishughulisha zaidi punde tu, alipoingia kwenye ndoa kwa sababu alifundwa mwiko kujibweteka kwa mume.

 

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Mwanaheri amesema watu wengi wanamshangaa zamani hakuwa kasi kwenye kusaka hela kama ilivyo sasa na ndiyo maana anawashukuru watu wazima waliomfundisha jinsi ya kuishi kwenye ndoa na inasonga mpaka leo.

“Unajua nilishika neno moja zuri kuwa, usiende kubweteka ukaja kuwa golikipa, basi toka hapo akili ilikuwa ikikimbia nifanye nini ili tu nisiwaangushe walionifunda na kweli nimefundika mpaka sasa, ni mmoja wa wafanyabiashara wazuri,” alisema Mwanaheri.Toa comment