Mwanamke mjamzito amuokoa mume wake baada ya kushambuliwa na papa (+Video)

2 0

Mwanamke mja mzito aliogelea baharini katika eneo la Florida kumuokoa mumewe kutoka kwa shambulio la papa.

Maafisa wa polisi walisema kwamba Andrew Charles Eddy 30, alikuwa akiteleza baharini kwa kutumia ubao katika eneo la Sombrero lakini akaumwa na papa mara tu alipoingia baharini.

”Mkewe aliuona mgongo wa papa huyo huku damu ya mumewe ikianza kutapakaa baharini na kuruka baharini bila kusubiri”, maafisa wanasema.

Baada ya kumuokoa mumewe na kumpeleka eneo salama ndugu zake wengine walipiga simu kwa 911 kupata usaidizi. Alisafirishwa kwa ndege hadi katika kituo cha kukabiliana na majeruhi ambapo alitibiwa jeraha baya la bega.

Afisa wa uokozi Ryan Johnson aliambia vyombo vya habari kwamba bwana Eddy alikua katika hali mbaya wakati alipowasili.

Wanandoa hao kutoka jimbo la Georgia , walikuwa katika likizo katika jimbo la Florida na familia na walikuwa wakisafiri kwa kutumia boti la kibinafsi pamoja.

Baadhi yao walikuwa tayari wakiteleza baharini kwa kutumia ubao wakati bwana Eddy alipoingia baharini kujiunga nao.

Naibu Christopher Aguanno aliandika katika ripoti ya polisi kwamba kulikuwa na watu wengine wasiotoka katika kundi lao waliokuwa wakiteleza kwa ubao baharini.

Mashahidi baadaye waliripoti kumuona papa mkubwa mwenye urefu wa futi 10 akiogelea katika eneo hilo mapema siku hiyo.

Florida ina idadi kubwa ya mashambulizi ya papa duniani, huku visa 21 vikiripotiwa 2019 kulingana na makavazi ya Florida .

Hatahivyo mashambulizi ya papa duniani ni machache.

Posted from

Related Post

Dereva Mlevi Aua Wanawake Watatu

Posted by - November 11, 2019 0
Dereva Mlevi Aua Wanawake Watatu November 11, 2019 by Global Publishers Jeshi la Polisi mkoani Arusha linamshikilia dereva wa gari…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *