Mwanamke wa kwanza kutoka Afrika kufanya kazi na shirika la Anga za juu ‘NASA’

2 0

Fadji Maina amekuwa mwanasayansi wa kwanza kutoka nchini Niger kufanya kazi na Shirika la Anga za Juu,NASA.

Bi maina mwenye umri wa miaka 29 alipata shahada ya uzamifu(PHD) mwaka 2016 na alijiunga na shirika hilo maarufu la anga za juu nchini Marekani mwisho wa mwezi uliopita.

Ameiambia BBC atatumia kazi yake mpya kurudishia shukurani sio tu nchi yake bali pia kwa bara zima la Afrika.

”Nawaasa wanawake wenzangu wasikate tamaa kufikia ndoto zao kwa sababu hakuna mtu angelifikiria mwanamke kutoka Niger, au msichana mdogo kutoka Niger, anataweza kufika mahali kama hapa. Siri ni kujiamini na kutafuta mazingira ambayo itakusaidia kufikia ndoto yako” alisema katika mahojiano yake na BBC.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *