Mwanza: Kichanga cha Wiki Mbili Chapotea Kimaajabu

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linachunguza tukio la kupotea katika mazingira ya kutatanisha kichanga cha wiki mbili ndani ya wodi ya akinamama waliojifungua kwa njia ya upasuaji katika hospitali ya Butimba ya wilaya ya Nyamagana mkoani humo.

 

Kichanga hicho chenye jinsi ya kike kinadaiwa kupotea baada ya mama yake mzazi Irene Juma ambaye ni Mkazi wa Serengeti mkoani Mara kwenda maliwatoni na aliporejea hakumkuta mwanaye kitandani hatua iliyomfanya apigwe butwaa.

 

Mganga Mkuu wa jiji la Mwanza Dk. Juma Mfanga ameeleza kusikitishwa na tukio hilo na kusema limeipaka matope hospitali hiyo.

 

Aidha, kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Muliro Jumanne Muliro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na juhudi za kumpata mtoto huyo zinaendelea.

CREDIT: ITVToa comment