Mwinyi Achukua Fomu ZEC ‘Tujipange’ – Video

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi amechukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea kiti hicho. Mwinyi amekabidhiwa fomu hizo na Jaji Mkuu (Mst.) Hamid Mahmoud Hamid mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

 

Akizungumza baada ya kuchukua fomu hizo, katika ofisi za ZEC, Dkt. Mwinyi amesema atahakikisha anaondoa matabaka ya kila aina, matabaka ya Upemba na Uunguja, Ukusini na Kaskazini na matabaka ya dini zote ili kujenga Zanzibar Mpya na kila mmoja kunufaika na maendeleo ya Zanzibar.

 

Aidha, Dkt. Mwinyi ametoa wito kwa wazanzibari wote kuhakikisha wanalinda amani na utulivu ili kufikia malengo ya kujenga Zanzibar Mpya itakayowanufahisha wazanzibari wote bila kubagua mtu.

 

“Iwapo mtanichagua kama kiongozi wenu ntahakikisha tunajenga uchumi wa kisasa na hivyo kufikia uchumi huo vijana muwetayali kuajiriwa popote ili kuinua uchumi wetu”, ameeleza Dkt. Mwinyi.

Dkt. Mwinyi amesisitiza kujenga miundombinu rafiki itakayo leta mazingira mazuri kwa wananchi hao ili kufikia uchumi wa kisasa na kunufaika na uchumi huo.

 

Katika hatu nyingine Dkt. Mwinyi amesema kuwa atahakikisha mapato yanakusanywa kwa ufasaha bila kupotea ili mapato hayo yakatekeleze miradi ya maendeleo kwa wananchi wa Zanzibar.

 

“Hivyo basi viongozi wa chama na wanachama wote sasa ni wakati wa kuingia kazini ili kuhakikisha chama kinapata ushindi katika uchaguzi huu kwani uchukuaji fomu ndo kiashiria cha kipenga cha uchaguzi kupulizwa rasmi”, amesisitiza Dkt. Mwinyi.

 

Dkt. Mwinyi ametamatisha kwa kuwataka wazanzibari wote kujitokeza siku ya kupiga kura Oktoba 28, mwka huu ili kuhakikisha chama kinapata ushindi kwa kishindo kikubwa. Toa comment