Mzamiru gari limewaka Simba – Gazeti la Dimba

5 0


NA MWANDISHI WETU

MAMBO yanaelekea kumwendea vizuri kiungo wa siku nyingi katika kikosi cha Simba, Mzamiru Yassin kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha tangu timu yake ilipoanza michuano ya Ligi Kuu Bara msimu huu.

Kiungo huyo ambaye kwasasa amekuwa akipewa nafasi kikosi cha kwanza, katika mechi nyingi amekuwa akidhihirisha uwezo wake kiasi cha kurejesha mapenzi kwa mashabiki.

Licha ya kucheza vizuri katika mechi karibu zote tatu ambazo timu yake imecheza, kiungo huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar ameshapachika mabao mawili.

Mzamiru alifunga bao lake la kwanza katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu, mchezo wa fungua dimba la michuano hiyo, kisha akafunga jingine wakati kikosi chake kikiivaa Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro na matokeo kuwa sare 1-1.

Kiungo huyo kwasasa anaungana na mwenzake ndani ya kikosi hicho, Clatous Chama, aliyekwishapachika mabao mawili katika mechi moja dhidi ya Biashara United.

Wengine waliokwishaweka kimiani mabao mawili kila mmoja ni Hassan Kabunda wa KMC, Prince Dube (Azam FC) na Reliants Lusajo (KMC).Source link

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *