Mzee Yusuf Ana Jambo Lake Dar Live

MWENYE Taarab yake Bongo; Mzee Yusuf, anatarajia kufanya bonge moja la shoo kwenye Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar.

 

Akizungumza na Risasi Jumamosi, muandaaji wa shoo hiyo, Rajab Mteta (KP) amesema, Septemba 25, mwaka huu pale Dar Live Mbagala, Mzee atakuwa na shoo hiyo maalum kwa ajili ya kutambulisha bendi mpya na wasanii wake, ambao imekuwa ni fumbo kwa mashabiki.

 

“Mashabiki wanaombwa kufika kwa wingi, kwani Mzee anatarajia kufanya makubwa. Baada ya shoo ya kukata na shoka ya Narudi Mjini, hii ya sasa itakuwa ni zaidi, maana ataenda kutambulisha bendi yake mpya na wasanii wapya, jambo ambalo limekuwa ni fumbo kwa mashabiki wa Taarab.

 

“Kiingilio kitakuwa ni shilingi 10,000 tu na kutakuwa na wasanii kibao ambao watamsindikiza Mfalme Mzee Yusuf, hivyo mashabiki wafike kwa wingi kwa ajili ya kupata burudani,’’ alisema KP.

 

KP alisema, muda wa burudani utakuwa ni kuanzia saa mbili usiku na mashabiki wanaombwa kuwahi mapema na ulinzi utakuwepo wa kutosha.

 STORI: HAPPYNESS MASUNGA, RISASI JUMAMOSIToa comment