Mzee Yusuf: “Kurudi Kwangu Mjini Kuna Mambo Mengi Sana” -Video

26 0Mzee Yusuf: “Kurudi Kwangu Mjini Kuna Mambo Mengi Sana” -Video

Mkurugenzi wa bendi ya Jahazi Modern Taarabu, Mzee Yusuf akifanya mahojiano na Global Radio.

IKIWA ni miezi kadhaa imepita tangu atangaze kurejea mjini, Mzee Yusuf ambaye pia hapo awali alikuwa mkurugenzi wa bendi ya Jahazi Modern Taarabu, hatimaye Julai 30, mwaka huu ana jambo lake zito pale Dar Live, Mbagala-Zakhem jijini Dar.

 

Akizungumza kupitia Global Radio Julai 15, 2020 katika ofisi za Global Group zilizopo Sinza jijini Dar es Salaam msanii huyo ambaye hapo awali aliamua kumgeukia mwenyezi Mungu hadi kufikia hatua ya kuwa Alhaj Mzee Yusuf, alisema kwamba watu wengi wanajiuliza anarudi mjini kufanya nini, lakini anaomba wawe wavumilivu kwani siku hiyo ndio ataweka wazi kila kitu.

“Kurudi kwangu mjini kuna mambo mengi sana, kwa sababu wote tunajua kwamba mjini ndio mambo mengi yalipo hivyo ukitaka kuwa shekhe haswaa unatakiwa uwe mjini, ukitaka kuwa mwizi kweli kweli ni mjini.

 

“Ukitaka kuwa msanii pia ni mjini yaani we anzia popote utakapoa anzia lakini mjini ndio kila kitu hivyohivyo na ukitaka kuwa mtangazaji mzuri lazima uwe mjini.

“Hivyo binafsi nimeona mjini kuna fursa, nimeona kuna kitu cha maana, kipo cha maana kwenye fursa, nilipohama mjini watu wengi walinipotea.

 

“Nimemkumbuka sana Fadha Mauji na Fatuma Nyoro lakini sijamkumbuka sana RJ kwa sababu yeye huwa anakuja sana kijijini kwetu kunisalimia, hivyo watu wakae mkao wa kula mfalme wa muziki wa Taarabu narudi mjini tarehe 30 mwezi huu pale Dar Live na ndio siku ambayo nitasema nimerudi mjini kufanya nini,” alisema Mzee Yusuf.

Stori: Memorise RichardToa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *