Mzungu Atangaza Saa 120 za Hatari Yanga

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mserbia, Zlatko Krmpotic, ametoa kauli ya kibabe akisema siku tano sawa na saa 120 zinamtosha kabisa kusuka kikosi kitakachocheza kwa kuelewana na kupata matokeo mazuri kwenye Ligi Kuu Bara.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache zimepita tangu kocha huyo aanze kazi rasmi ya kukinoa kikosi hicho alichokabidhiwa wiki iliyopita kwa ajili ya msimu huu wa 2020/21 Yanga inatarajiwa kuanza Ligi Kuu Bara Jumapili hii kwa kucheza dhidi ya Prisons kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Akizungumza na Spoti Xtra, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alisema katika kikao cha viongozi walichofanya na kocha, mwenyewe ameonekana kuridhishwa na viwango vya wachezaji wake wote.

 

“Kocha ameomba siku tano za kutengeneza muunganiko wa timu, lengo ni kuona wachezaji wanacheza kwa kuelewana ikiwemo kumiliki mpira na kutengeneza nafasi za kufunga.“Hizo siku tano ameziomba kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kabla ya kumalizia mazoezi ya mwisho Jumamosi timu iwe imeshaungana na kucheza kitimu ili kuhakikisha tunapata matokeo mazuri katika michezo ya awali,” alisema Mwakalebela

STORI: WILBERT MOLANDI, DARToa comment