Nataka kuoa wake 11 – Salongo Mayanja

3 0

Salongo Mayanja(Maniraguha) ni mganga wa kienyeji nchini Rwanda ambaye ameamua kufuata nyayo za baba yake kwa kuoa wanawake wengi.

Kwa sasa bwana Salongo Mayanja ana wake wanane na anasema anataka kuwa na wanawake 11 kama baba yake mzazi.

Anasema kuoa wanawake wengi ”ni raha isiyo na kifani ukiwa na uwezo kifedha”.

Pengine huenda unajiuliza anamudu vipi kutatua tofauti za kawaida zinazohusishwa na wake wenza?

Kujibu swali hilo na maswali mengine mengi mwandishi wa BBC Yves Bucyana alimtembelea Salongo Mayanja katika moja ya nyumba zake mjini Musanze kaskazini mwa Rwanda na kutuandalia makala haya.Musanze: Umugabo uzwi nka Dogiteri Salongo Mayanja yifuza kongeraho 4 mu  bagore 7afite – Ibazenawe.com

Salongo Mayanja, huwakutanisha wake zake wanane kila baada ya miezi mitatu

Mara kwa mara bwana Salongo huwakutanisha wake zake wanane ili kama njia ya kudumisha upendo kati yao.

”Hii ni siku maalumu isiyo ya kawaida kwa sababu wake wenza nimewatayarishia zawadi kwa ukarimu walionionesha” alisema.

Siku hiyo maalum kila mke anaonekana mwenye furaha. Mmoja wao ambaye ndiye mke mdogo, aliolewa na Salongo wiki mbili zilizopita

”Nilikuwa na mchumba mwengine.Lakini mwishowe nilimkatia na kukubali kuolewa na huyu Bwana licha ya kwamba nilijua ana wake wengine wengi” anamsimulia mwandishi wa BBC.

Familia ya bwana Salonga hujumuika kila baada ya miezi mitatu kwa mwaliko wake ambapo wanasherehekea pamoja na kupeana zawadi.Wake wa Salongo Mayanja

Wake wa Salongo Mayanja wakipokezana zawadi katika moja ya mkutano wao wa kila baada ya miezi mitatu

Wakati baadhi ya watu wanaona kwamba ni mzigo mkubwa kuoa na kutunza zaidi ya mke mmoja kutokana na hali ya maisha inavyozidi kuwa ngumu,Lakini yeye anasema kuishi na wake wengi ni raha.

”Naishi nao vizuri kuliko mtu aliye na mke mmoja ambapo unakuta wanaishi kwa ugomvi usiokwisha”

Pia anaongezea kusema kuwa anasaidia serikali kutunza hawa wanawake sababu kila mke wangu niliyemuoa ”anasaidia pia familia yake yote” kwasababu ana uwezo.

”Kila mwanamke ana shamba nanyumba yake kiasi kwa hatahangaika yeye na watoto wake mimi nitakapokuwa sipo” aliendelea kusema kwa madaha.

Wake zake wenyewe wanasema wanaishi pamoja vizuri bila mtafaruku wowote wala wivu kama anavyosimulia mmoja wao Uwanyirigira Jeanne D’Arc.Wake wa Salongo Mayanja

”Mimi ni mkewe wa tatu,niliolewa nikijua wazi kwamba mimi siye mkewe kwa kwanza.sina wasi wasi wa mstakabali wa watoto wangu kama bwanangu hatakuwepo, kwani kila mkewe ana nyumba yake na mashamba yake”

”Tunavyoishi sasa kuna mke mmoja anayehusika na mahitaji yetu kama mavazi,viatu au vifaa vya nyumbani na mke wa kwanza ndiye anayeshughulikia masuala ya chakula kwa sisi sote”

Salongo Mayanja, mwenye umri wa miaka 42, manusura wa vita vya Rwanda vya mwaka 94 na askari mstaafu.

Ana watoto 14, kila mke akiwa na watoto wawili.

Rwanda hairuhusu ndoa ya mke zaidi ya mmoja na wala sio kosa la jinai.

Lakini kunapotokea kesi inayohusisha na mahusiano na ukewenza, haki hupewa mke mkubwa na watoto wake.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *