NBC Bank Yawagusa Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum Chalinze

4 0NBC Bank Yawagusa Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum Chalinze

Meneja wa Benki ya NBC tawi la Samora Bi Zubeider Haroun (kulia) akimshukuru  Mwalimu Mkuu Msadizi wa Shule ya Msingi Chalinze Bi Aufemia Ngweta (kushoto) wakati wa kukabidhi Msaada wa Mifuko ya saruji iliyotolewa na Benki ya NBC kwa kushirikiana na Umoja wa Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kwa ajili ya kuboresha Miundombinu ya Vyoo kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum shuleni hapo. 

Chalinze, Pwani: September 21, 2020: Wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi ya Chalinze mkoani Pwani wamehimizwa kusoma kwa juhudi ilikutengeneza maisha yao ya baadaye huku wakipewa changamoto ya kujitahidi kilawakati kuwa bora katika masomo yao na kwa kila kitu wanachofanya.

 

Hamasa hiyo imetolewa mapemawiki na Meneja wa Benki ya Kitaifa ya Biashara (NBC) Tawi la Samora Bi ZubeiderHaroun wakati akikabidhi mifuko 75 ya saruji kwa shule hiyo ikiwa ni hatua yabenki kuboresha miundombinu shuleni hapo hususani kwa kujenga choo chawanafunzi wenye mahitaji maalum.

 

 

Bi Zubeider aliwasihiwanafunzi hao kuwa elimu inaweza kuwapeleka mbali na kutimiza ndoto zao, kwa hivyowanahitaji kusoma kwa juhudi katika masomo yao huku akiwasisitiza kutokatatamaa hasa wanapopata changamoto katika safari zao za masomo.

 

“Kwa hivyo nawasihi muwekejuhudi katika masomo yenu ili kwa ajili ya faida ya maisha yenu ya baadae kwa kuwa elimu ni ufunguo ambaounafungua milango ya maisha yote. ” alisisitiza

 

Aliongeza kuwa benki hiyoitaendelea kusaidia maendeleo ya Elimu na ikiwemo kwa wale walio na mahitajimaalum ili kuboresha mfumo wa elimu jumuishi nchini.

 

Meneja wa NBC tawi la Samora Bi Zubeider Haroun akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi mifuko ya saruji iliyotolewa na Benki hiyo kwa kushirikiana na Umoja wa Wanafunzi wa Chuo cha Udhibiti wa Fedha (IFM). Msaada uliotolewa utasaidia kuboresha miundombinu katika Shule hiyo hasa jengo la Vyoo vya wanafunzi wenye mahitaji maalum.

 

“Kama benki tumejitolea kabisa kusaidia ujenziwa hitaji hili muhimu la miundombinu ya katika shule hii ili kuboreshaupatikanaji wa elimu hususani kwa wanafunzi wenye uhitaji maalum.’’ Alisema.

 

Pia, Bi Zubeider alitoa witokwa taasisi zingine na watu binafsi kuchangia kwa shule na vituo vya elimu kamanguzo muhimu kuelekea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

 

Akipokea msaada huo BiAufemia Ngweta, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo aliishukuru Benki ya NBCkwa msaada huo na utashi wake katika kusaidia ukuaji wa elimu katika Wilayahiyo. Pia alitoa wito kwa wadau zaidi kusaidia shule hiyo.

Maofisa wa  benki ya NBC tawi la Samora wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Chalinze na Wawakilishi wa Umoja wa Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) walipokwenda kukabidhi msaada wa mifuko ya saruji kwa ajili ya Ujenzi wa Vyoo kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum shuleni hapo.  

 

“Hapa shuleni kunawatoto wenye ulemavu tofauti, kuna wale walio na ugonjwa wa kupooza kwa ubongoambao wanahitaji vifaa vingi vya kuchangamsha akili zao ili waweze kujifunzavitu mbalimbali kama ufundi na ujuzi mwingine kwa maendeleo yao ya baadaye. Kwahivyo juhudi zaidi zinahitajika kuhakikisha tunawafundisha vyema. ”Bi Ngwetaalifadhaika

 

Alimshukuru pia Bi Zubeidakwa kuwahamasisha wanafunzi hao, akibainisha kuwa ni matumaini yake wanafunzihao  watabadilisha mawazo yao nakuthamini kwamba watu wenye mahitaji maalum wanaweza kuishi na kufaulu maishanihususani kupitia elimu.

 

Wanafunzi wa Shule ya Msingiya Chalinze walishukuru Benki hiyo kwa msaada huo huku wakiaahidi kufanyavizuri kitaaluma sambamba na kutoa wito kwa jamii iendelee kuwasaidia iliwaweze kutimiza ndoto zao.

 

 

 Toa comment

Posted from

Related Post

Kocha wa Simba Akimbilia TFF

Posted by - April 9, 2020 0
Kocha wa Simba Akimbilia TFF April 9, 2020 by Global Publishers KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck, ni kama…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *