Ndege ya Iran yaanguka Barabarani ghafla, baadhi ya abiria watokea dirishani(+Video)

16 0

Ndege ya abiria nchini Iran imedondoka Barabarani baada ya kuteleza wakati ikitua uwanja wa ndege.

Kwa mujibu wa maafisa wa afya, abiria wawili kati ya 136 waliyokuwemo kwenye ndege hiyo wamepata majeraha.

Ndege hiyo ya kampuni ya Caspian iliondoka mjini Tehran. Matairi yake hayakujitokeza kabisa wakati ilipotarajiwa kutua.

Picha za abiria waliokuwa wakitoka katika ndege hiyo zilichapishwa katika mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Runinga ya serikali ilinukuu maafisa wa usafiri wa angani wakisema kwamba rubani aliishusha ndege hiyo kuchelewa hivyobasi akakosa barabara ya ndege.

Ripota mmoja ambaye alikuwa ndani ya ndege hiyo alisema kwamba matairi ya nyuma ya ndege hiyo yaliharibika na kwamba ndege hiyo iliteleza bila matairi yake.

Msemaji wa shirika la udhibiti wa safari za angani Reza Jafarzadeh aliambia chombo cha habari cha Isna news kwamba ndege hiyo iliteleza kutoka katika barabara yake siku ya Jumatatu alfajiri .

Aliongezea kwamba uchunguzi unaendelea.

Iran ina rekodi mbaya ya safari za ndege . Watu 66 walifariki katika ajali ya ndege mnamo mwezi Februari 2019, huku makumi wakifariki 2019 wakati ndege ya IranAir ilipovunjika vipandevipande baada ya kuanguka 2011.

Muungano wa Ulaya umepiga marufuku kampuni mbili za ndege kutotumia anga yake kutokana na wasiwasi wa kiusalama.

Iran ilikuwa imepanga kuimarisha ndege zake zilizozeeka baada ya vikwazo vya miaka mingi kuondolewa ikiwa ni miongono mwa makubaliano ya mkataba wa kinyuklia wa 2015 na mataifa yenye uwezo mkubwa.

Hatahivyo wizara ya fedha nchini Marekani ilifutilia mbali leseni ya kampuni kuuzia Iran ndege za abiria baada ya rais Donald Trump kujiondoa katika makubaliano hayo 2018.

Posted from

Related Post

CUF Yatangaza Wagombea Ubunge 136

Posted by - August 24, 2020 0
CUF Yatangaza Wagombea Ubunge 136 August 24, 2020 by Global Publishers Chama Cha Wananchi (CUF) nchini Tanzania, kimetoa orodha ya…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *