Ndege Yaanguka Serengeti, Yaua Watanzania Wawili

6 0

Ndege ndogo ya Shirika la Auric Air imepata ajali leo Jumatatu asubuhi Septemba 23, 2019 katika uwanja mdogo wa ndege eneo Seronera ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania.

 

Ajali hiyo imetokea saa 1:30 asubuhi ambapo ilikuwa ikiruka kutoka Serengeti kwenda Arusha baada ya kushusha watalii.

Katika ajali hiyo, rubani na abiria mmoja wamefariki dunia.

Kamishna Msaidizi mwandamizi wa shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Pascal Shelutete amethibitisha kutokea ajali hiyo.

“Tunatoa taarifa zaidi baadaye kwani sasa kazi inayoendelea ni kuokoa vitu na kuhifadhi miili,” amesema.

Posted from

Related Post

Polisi Wala Bingo Kutoka NMB

Posted by - September 26, 2019 0
Polisi Wala Bingo Kutoka NMB September 26, 2019 by Global Publishers BENKI ya NMB, imewahakikishia askari wa Jeshi la Polisi…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *