Ndemla, Ajib kuwatenganisha ufanye kazi

6 0


NA WINFRIDA MTOI
WACHEZAJI wa Simba, Ibrahim Ajib na Said Ndemla, hakuna anayeweza kutibua urafiki wao kutokana na vile walivyoshibana na muda mwingi wanaonekana wako pamoja.

Hata katika mazoezi ya timu hiyo, yanayofanyika viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam, wachezaji hao wamekuwa na utaratibu wa kupaki magari yao sehemu moja na wakiondoka wanaongozana, kama ataanza Ajib, ujue Ndemla yupo nyuma.

Licha ya kuishi maeneo tofauti, Ajib Tabata na Ndemla Sinza, lakini wanapomaliza mazoezi, lazima wasubiriane waondoke kwa pamoja tena muda mwingine huwa wa mwisho kutoka eneo hilo.

Jina la utani ambalo Ndemla hulitumia kumuita Ajib wanapokuwa wanapiga stori zao, anamuita Mwinyi.


Source link

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *