Nisha Aeleza Corona Ilivyoam-Kwamisha

MSANII wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amefunguka Virusi vya Corona vilivyomkwamisha kibiashara, kwani ameshindwa kusafiri kwenda nchini China.

 

Akistorisha na Amani, Nisha alisema amezoea kusafiri kwenda nchini China kuchagua nguo za biashara mwenyewe lakini kwa sasa kutokana na tishio hilo hatari la Corona, ameshindwa kusafiri.

“Kiukweli Corona imenikwamisha sana kibiashara maana huwa naenda China kuchagua nguo zangu za biashara mwenyewe, namuomba Mungu aondoe janga hili duniani maana linaturudisha nyuma mno,” alisema Nisha.
Toa comment