Nitamshauri Rais avunje bunge- Jaji Maraga – Dar24

6 0

Jaji mkuu wa Kenya David Maraga ameeleza kumshauri Rais wa kenya Uhuru Kenyeta kuvunja bunge la nchi hiyo baada ya kushindwa kupitisha sheria inayowatambua watu wanaozaliwa na jinsia mbili.

CJ Maraga ,katika hatua yake ambayo haijawahi kutokea hapo awali, amesema kwamba bunge limekataa kufuata agizo la mahakama kuu , la kutunga inayotambua watu wenye jinsia mbili kwa zaidi ya miaka 9.

“haiwezekani kwamba Bunge alijatii agizo la Mahakama kuu katika maombi ya kikatiba No. 371 ya 2016 . kwa zaidi ya miaka 9 sasa bunge halijatunga sheria inayohitajika kutekeleza sheria ya jinsia mbili ambayo ,kama korti ya rufani ilivyozingatia katika uamuzi wake ,ni dhahiri bunge halijali mtazamo kuhusu jambo hili,”alisema Rais Uhuru.

Kama matokeo ,jaji mkuu amesema kwa kuzingatia katiba inayompa mamlaka kumshauri rais kuvunja bunge nae atafanya hivyo .

“ikiwa bunge litashindwa kutunga sheria kwa mujibu wa agizo chini ya kifungu cha (6) (b) , Jaji mkuu atamshauri Rais atavunja bunge,Ni jukumu langu kikatiba kukushauri rais wa jamuhuri ya kenya ,ambayo ninafanya hivi kulivunja bunge” alisisitiza Jaji Maraga.

Hatua hii ya jaji kumshauri Rais kuvunja bunge itakuwa ni mara ya kwanza kutokea hasa kwa nchi za afrika , na ikumbukwe kuwa 2015  Jaji Maraga aliandika historia ya kutoa uamuzi ya kurudiwa uchaguzi mkuu wa kenye baada ya mvutano kutokea katika duru ya kwanza ya uchaguzi .

Akamatwa akipeleka sumu Ikulu – Marekani

Comments

comments

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *