Nyani aiba smartphone, ajishuti video na kujipiga picha za ‘Selfie’ (+Video)

1 0

Mwanafunzi mmoja raia wa Malaysia amepata picha za selfie za tumbili na video kadhaa katika simu yake iliyokuwa imepotea.

Picha hizo zimesambazwa sana mitandaoni tangu Zackrydz Rodzi ilipoiweka kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Zackrydz, 20, ameiambia BBC kwamba aligundua simu yake imepotea alipoamka usingizini, na alipojaribu kupiga simu yake aliisikia ikilia katika kichaka karibu na ua lao, na hapo ndipo aliona simu iliyokuwa kwenye matope chini ya mnazi.

Alipofungua akagundua nyani alikuwa mhusika na ushahidi wake ulimshtua.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *