Nyosso Jeshini, Ngassa Daraja la Kwanza Ndanda FC

ALIYEKUWA beki wa zamani wa klabu za Simba, Coastal Union, Mbeya City na Kagera Sugar, Juma Said ‘Nyosso’ amesalia kwenye Ligi Kuu Bara msimu ujao na safari hii ataonekana akiwa na Ruvu Shooting.

 

Mkongwe huyo amejiunga Ruvu kama mchezaji huru akitokea Kagera baada ya mkataba wake kumalizika wa kuendelea kukipiga hapo baada ya klabu yake hiyo kutangaza kuachana naye.

 

Wakati Nyosso akibakia, kiungo mshambuliaji mkongwe Mrisho Ngassa naye ametimkia Ndanda FC ya Mtwara itakayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kwenye msimu ujao.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano na kuthibitishwa na Nyosso zinaeleza kuwa amejiunga na Ruvu kama mchezaji huru baada ya kufikia makubaliano mazuri kabla ya kusaini mkataba wa miezi sita.

 

“Ni kweli msimu ujao nitaonekana nikiwa na Ruvu ni baada ya kufikia mazungumzo mazuri kati yangu na uongozi wa timu hiyo, nimesaini mkataba wa miezi sita pekee.

 

“Zilikuwepo klabu nyingi zilizoonyesha nia kubwa ya kunisajili kabla ya kuchukua maamuzi ya kusaini Ruvu,”alisema Nyosso.Kwa upande wa Ngassa mwenyewe alisema kuwa “Hizo taarifa za kweli, nimerudi kwenye timu yangu ya zamani ya Ndanda niliyowahi kuichezea baada ya kufikia makubaliano mazuri kati yangu na viongozi.

 

”Wachezaji wengine wakongwe waliosajiliwa na Ndanda ni Paul Ngalema, William Lucian ‘Gallas’ , Stamili Mbonde na Henry Joseph Shindika.Toa comment