Nyota namba moja wa Tenis Djikovic atolewa kwenye michuano ya US OPEN kwa kumpiga refa na mpira (+Video)

7 0

Djokovic alikua akikabiliana na Pablo Carreno Busta ambapo alikua ameshapoteza seti ya ufunguzi kwenye uwanja wa Arthu Ashe huko Marekani.

Raia huyo wa Serbia aligonga mpira nyuma yake kwa kuchanganyikiwa na ukampiga jaji wa kike na baada ya tukio hilo Djokovic alikimbia kuangalia hali ya jaji huyo ambaye alikua ameumia.

Mwamuzi wa mashindano Soeren Friemel alijitokeza na kuzungumza na Mwenyekiti wake Aurelie Tourte na Andreas Egli ambaye ndiye alikua  msimamizi wa mchezo ambapo walifanya mazungumzo marefu na Dkokovic kabla ya kutoa maamuzi.

Aliaomba kwa muda mrefu kuwa haikua makusudi lakini baada ya uamuzi kutolewa aliondoka uwanjani.

Djokovic atakumbana na faini nyingine kwa kutofanya mkutano na waandishi wa habari kama utaratibu ulivyo vilevile alama zake alizovuna tangu kuanza kwa michuano zitafutwa ambazo zingeweza kumuimarisha kwenye viwango vya ubora.

Picha zinaonyesha Djokovic aliondoka kwenye gari yake .

Mpaka anafikia raundi ya nne ya mashindano hayo Djokovic alikua ameshinda michezo 25 mfululizo tangu kuanza kwa mwaka 2020.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *