Ostadh Juma Afunguka Kuhusu Kufilisika

Meneja Ostadh Juma na Musoma amefunguka madai ya wasanii kumfilisi hadi kupelekea kuhama Jijini Dar Es Salaam na kuhamia Jijini Tanga, pia amesema asili ya watu wa Musoma wanafanya muziki kama starehe ila sio biashara.

 

Ostadh Juma ameeleza kuwa; “Wasanii hawajawahi kunifilisi kwanza sanaa ya muziki nilikuwa nafanya kama starehe kwangu na ukiangalia asili ya watu wa Musoma wengi wao wanafanya muziki kwa starehe na sio biashara kwa sababu mimi hakuna pesa ya muziki ambayo nimewahi kula ila nimetumia pesa nyingi kusimamia muziki.

 

Aidha, Ostadh Juma na Musoma ameongeza kusema sio kwamba amefilisika ndiyo amehamia Tanga bali ameenda kwa ajili ya masomo, pia kabla ya kuja Dar es Salaam alipitia mkoani humo na ndipo alipopewa jina la Ostadh.

 

“Namjua Dogo Janja nimekaa naye kwa muda mrefu ni mwanangu kabisa namjua kuliko hata Madee, kiatu anachovaa Dogo Janja Madee hawezi kuvaa, sasa hapo nani ambaye anaweza kumsimamia mwenzake. 

 

“Young Killer ni msanii mkubwa sana nimewahi kufanya naye kazi yuko vizuri kuliko watu wanavyomuona, pia sio msanii wakubahatisha kwenye kazi.

 

“Nikimzungumzia Juma nature kiukweli ni msanii ambaye ana msongo wa mawazo katika maisha yake, siwezi kufanya nae kazi tutasumbuana,” amesema Ostadh Juma.Toa comment